Ufafanuzi wa baadhi ya istilahi katika dhana ya viambishi vya vitenzi. k.m.
- Mzizi- Ni sehemu ya kitenzi ambayo haibadiliki katika kunyambua/kubadilisha muundo wa vitenzi. k.m.
a-na-pik-a, a-na-m-pik-i-a, ki-na-pik-ik-a
- Ambisha- Ni kuongezwa viambishi vya vitenzi kwa hivyo huongezwa kwa vitenzi(mizizi). k.m.
a-na-pik-a
viambishi kiambishi
- Viambishi Awali-Hivi ni viambishi vinavyoambishwa kabla ya mzizi
- Viambishi Tamati - Hivi ni viambishi vinavyoambishwa baada ya mzizi. k.m. a-na-pik-a v. awali v. tamati