Skip navigation

UTANZU WA MAZUNGUMZO: MAAPIZO

MAZUNGUMZO

  • Maongezi ya mdomo yenye usanii.

  • Utanzu huu una vipera vifuatavyo:

  • soga

  • malumbano ya utani

  • mawaidha

  • hotuba

  • ulumbi

  • maapizo

Maapizo

  • Maombi maalum ya kumtaka Mungu, miungu au mizimu kumwadhibu mhusika hasidi, mkinzani au muovu.

Sifa za maapizo

  • Yalitolewa kwa waliokwenda kinyume na matarajio ya jamii.

  • Yalifanywa mahali maalum k.v. makaburini, porini, chini ya miti mikubwa, n.k.

  • Hutolewa kwa ulaji kiapo.

  • Yalitolewa na mwathiriwa au watu maalum walioteuliwa.

  • Maapizo huaminiwa yataleta maafa kwa jamii.

Umuhimu wa maapizo

  • Kuonya na kutahadharisha wanajamii dhidi ya maovu.

  • Kutambulisha jamii kwani kila mojawapo ina aina yake ya kuapiza.

  • Kukuza umoja katika jamii kwani kaida na miiko hufanya wanajamii kujihisi kuwa kitu kimoja.

  • Kuadilisha wanajamii kwa kujifunza kutenda mema ili kuepuka laana.

Mfano

Ikiwa kweli wewe ni mkazamwanangu,

Nami ndiye nilompa uhai mwana unoringia,

Anokufanya upite ukinitemea mate,

Chakula kuninyima, wajukuu kunikataza ushirika,

Miungu nawaone chozi langu, wasikie kilio changu,

Mizimu nawaone uchungu wangu,

Radhi zao wasiwahi kukupa,

Laana wakumiminie,

Uje kulizwa mara mia na wanao,

Usiwahi kufurahia hata siku moja pato lao,

Watalokupa likuletee simanzi badala ya furaha,

Wakazawanao wasikuuguze katika utu uzima wako!