Skip navigation

JUKUMU 1

Mfano1

Ikiwa kweli wewe ni mkazamwanangu,

Nami ndiye nilompa uhai mwana unoringia,

Anokufanya upite ukinitemea mate,

Chakula kuninyima, wajukuu kunikataza ushirika,

Miungu nawaone chozi langu, wasikie kilio changu,

Mizimu nawaone uchungu wangu,

Radhi zao wasiwahi kukupa,

Laana wakumiminie,

Uje kulizwa mara mia na wanao,

Usiwahi kufurahia hata siku moja pato lao,

Watalokupa likuletee simanzi badala ya furaha,

Wakazawanao wasikuuguze katika utu uzima wako!

Mfano 2

kwa kweli dunia haini. mtoto mdogo kafanyiwa tendo la kinyama la ubakaji kisha dhulumati

wake kumfunga kwa kamba kumwacha kaka tu!kama wazee wa kijiji hiki tunakilaani kitendo hiki na

tunawapa muda wa siku ya leo kujisalimisha kwetu kuomba msamaha la sivyo,kesho

asilione anga la jua

Miungu yetu ivilaani vizazi vyao, vipatwe na laana,

siku zote wakumbwe na maafa.