Skip navigation

KAZI 3

MNYAMBULIKO WA VITENZI

MNYAMBULIKO WA VITENZI

Kunyambua ni kurefusha

Kunyambua kitenzi ni kukirefusha kwa kuvipa /kuviongeza viambishi katikati ya mzizi na viishio. Minyambuliko yote huanzia kwa vitenzi kuwa katika hali ya kawaida /hali ya kutenda /hali ya kufanya.

Mifano

Mzizi                 kiishio

Pig-                 a

Chez -              a

Lim-                 a

Kimbi-             a

Jinsi ya kunyambua vitenzi

 

Vitenzi hunyambuliwa katika jinsi mbalimbali ;

Kauli ya kutendea               kauli ya kutendatenda

Kauli ya kutendewa            kauli ya kutendama

Kauli ya kutendeka             kauli ya kutendata

Kauli ya kutendesha           kauli ya kutendua

Kauli ya kutendeshea         kauli ya kutenduka

Kauli ya kutendeshwa        kauli ya kutendana

 

Tanbihi ;si vitenzi vyote ambavyo hunyambuliwa katika hali zote.

Kawaida                  kutendea                       kutendesha

Pig.a                        pigia                              pigisha

Chez.a                     chezea                            chezesha

l.a                            lia                                   lisha

f.a                           fia                                   fisha

to.a                        tolea                                 toza

imb.a                    imbia                                imbisha

tembe.a                    tembelea                         tembeza

li.a                        lilia                                      liza

1.kauli ya kutenda/kufanya/kawaida

hivi ni vitenzi ambavyo havijaongezewa viambishi vyovyote vya tamati isipokuwa kiishio  -a.

kiishio –a si sehemu ya mzizi wa kitenzi kwa vile ni kawaida kwa vitenzi vya Kiswahili vyenye asili ya kibantu kuishia kwa herufi –a katika hali yakinishi.

Vitenzi hivi ndivyo msingi wa kunyambua vitenzi vyote.

Mifano

Tembe.a                 kop.a

Simam.a                 end.a

Chom.a                  twa.a

Shik.a                    kos.a

Ingi.a                     chap.a

2.kauli yakutendea/kufanyiwa

Kauli hii huwakilishwa kwa viambishi hivi;

-e-        -li-

-i-        -le-

Mifano

Kawaida                             kutendea

li.a                                        lilia

tembe.a                                tembelea

kos.a                                     koselea

end.a                                    endea

choma                                 chomea

chap.a                                  chapia

lal.a                                       lalia

l.a                                        lia

o.a                                       olea

kasirik.a                               kasirikia

to.a                                      tolea

sentensi

mtoto alimlilia mama.

Abdala amemlia mtoto chakula.

Amenipigia mpira.

Nalia mikono.

Babu anatembelea mkongojo.

Maelezo

Mtoto alilia kwa sababu pengine mama alimwacha, hakumnyonyesha, alitaka abebwe n.k

Msemaji ala kwa kutumia mikono.kauli hii hivyo basi hutumiwa kuonyesha jinsi au kifaa kinachotumiwa kutendea jambo.

Abdala amekula chakula badala ya mtoto kukila hicho chakula.

Amenipiga kwa kutumia mpira. {ala/kitumizi}

Amenipiga kwa sababu pengine nimeupoteza mpira wake,nimeutoboa n.k

Ameupiga mpira unielekee .{kunitolea pasi}

Ameupiga kwa niaba yangu vile pengine nina jeraha.

Mkongojo ni kifaa kinachomsaidia babu kutembea.

Aidha kauli hii huweza kuonyesha kuwa kitendo kilitendewa mahali Fulani. Mifano

Askari alimshikia uwanjani

Nilivalia nguo chumbani mwangu.

Serikali iliwazuilia mateka wapi?

3 kauli ya kutendwa na kutendewa

Kauli hizi huwakilishwa na viambishi hivi;

-ew-                    -lew-                -liw-

-w-

                     Mifano ya vitenzi

 

vitenzi

kutendwa

kutendewa

Chez.a

chezwa

Chezewa

Imb.a

imbwa

Imbiwa

Lim.a

limwa

Limiwa

f.a

©

Fiwa

l.a

©

Liwa

Ch.a

©

Chiwa/chewa

j.a

©

Jiwa

Chw.a

©

Chwewa

Chor.a

chorwa

Chorewa

Tobo.a

©

Tobolewa

Chom.a

chomwa

Chomewa

Kat.a

katwa

Katiwa

Le.a

©

Lelewa

Bomo.a

©

Bomolewa

Pak.a

pakwa

Pakiwa

Anguk.a

©

Angukiwa

 

Kauli hizi huonyesha;

Kwamba kitu Fulani kimetendewa kitendo na kimeathirika moja kwa moja.

Watoto waliimbiwa wimbo mzuri na mwalimu wao.-wimbo mzuri uliimbwa na mwalimu kwa watoto.

Ukuta unapakwa rangi ya kijani kibichi.

3.Kauli ya kutendesha/ kufanyisha.

Huonyesha kuwa kitendo kimesababishwa na mtu au kitu Fulani.

Ina viambishi mbalimbali;

-esh-          -ish-              -lesh-                 -lish-                       -sh-           -ez-          -iz-

-lez-           -liz-              -fy-                    -vy-                          -s-               -z-      

 

 

Mifano

Cheza  -    chezesha            ruka     -       rusha                         ig.a     -   igiza

Lima    -     limisha              takat.a    -    takas.a                       tok.a  -      tokeza

Pon.a   -        ponya               ogop.a   -    ogofya                      lew.a       -levya

Shuk.a     - shusha                 tikita       -tikisa                            toroka     -torosha

Kos.a       -kosesha                shuka   -    shusha                        chemk.a  -     chemsha

Va.a     -visha                       wez.a         -wezesha

Sentensi

Dereva aliwashusha abiria kituoni.

Simba huwaogofya watu wengi.

Dawa za kulevya zimewaathiri vijana.

Nguo zimefuliwa na sasa zinatakasa.

4.kauli ya kutendeka /kufanyika

Huonyesha; a) kuwa kitendo kimetendeka na kimetimilika bila kuonyesha mtendi wake au kilichohusika .

Mfano    kikombe kimevunjika.

Haijulikani mtu aliyekivunja wala kitu kilichokivunja kikombe.

b)uwezekano wa mtu/ kitu Fulani kupatwa na tukio fulani katika hali ya uyakinisho.

Mfano,  machungwa haya yanalika.

Maana ni kuwa kuna uwezekano wa kuyala machungwa hayo.

Viambishi vya kauli hii ni;

-ik-                 -lek-            -lik-              -ikan-

 

 

vitenzi

Kauli ya kutendeka

twaa

twalika

kaa

kalika

chukua

chukulika

vunja

vunjika

noa

noleka

pata

Patika/patikana

taka

Takika/takikana

kopa

Kopeka

tega

Tegeka

samehe

Sameheka

osha

Osheka

vaa

Valika

vua

Vulika

 

vitenzi

Kauli ya kutendeka

Funga

fungika

Fungua

funguka

Imba

imbika

Pita

pitika

Cheza

Chezeka

Lima

Limika

Pasua

Pasuka

Rarua

Raruka

Toa

Toka/toleka

Nyoa

Nyoleka

Ng’oa

Ng’oleka

Soma

someka

Nena

neneka

Tia

tilika

 

MATUMIZI

Nimemaliza kuutega mtego. (kawaida)

Mtego umetegeka.

Niliuosha mkoba wangu.{kawaida}

Mkoba uliosheka./mkoba wangu uliosheka.

Baba alivaa shati lake.{kawaida}

Shati lilivalika.

Mtoto  anataka maziwa.{maziwa yanatakikana}

 

 

 

  1. kauli ya kutendana

Huleta maana kuwa mtu mmoja ametenda jambo kwa mwingine na huyo mwingine akatenda jambo hilo kwa aliyemtendea.

Kitenzi katika kauli hii lazima kihusishe mashiriki zaidi ya mmoja.huwakilishwa na –an-

Kitenzi

Kauli ya kutendana

Pig.a

pigana

Suk.a

sukana

Kut.a

kutana

On.a

onana

Vut.a

vutana

Teg.a

tegana

 

Sentensi

Simba na chui wanaogopana.

Mbabekazi na Kikubi wamezoea kubishana.

Sote tulielezana mikasa iliyotusibu.

Mnyamuliko wa vitenzi vyenye silabi moja

kitenzi

kutendea

kutendeka

kutendesha

kutendana

kutendewa

Ch.a

chea

©

©

©

chewa

Ch.a

chia

chika

chisha

chana

chiwa

f.a

fia

©

fisha

fana

fiwa

j.a

Ji.a

jika

©

©

jiwa

l.a

lia

lika

lisha

lana

liwa

p.a

pea

peka

pesha

pana

pewa

Ny.a

Nyia/nyea

©

nyesha

©

Nyiwa/nyewa

Nyw.a

nywea

nyweka

nywesha

©

nyewa

Pw.a

©

©

©

©

©

Pa.a

palia

palika

paza

©

paza

Pa.a

palia

palika

©

©

paza

Lal.a

lalia

lalika

laza

©

laliwa

w.a

wia

wika

wisha

©

 

Ch.a      chomoza kwa jua.

            Kuwa na woga.

Ny.a      enda haja kubwa

            Toa kitu cha majimaji ama nyauka .

w.a       tokea/tendeka/fanyika

pw.a     toka kwa maji ufuoni na kwenda mpaka sehenu ya mbali ya bahari.

f.a        tokwa na uhai /kata roho

           ishiwa na nguvu

          kupenda kupita kiasi

          kuwa katika hali ya kutoendelea

          kufikia mwisho

pa.a     ondoa mamba ya samaki

           enda juu

           chukua makaa kutoka kwenye jiko

                             Matumizi

mama ameyanywa maziwa ya mtoto.{kutenda}

maziwa ya mtoto yamenywewa na mama.{kutendewa}

mtoto amenywewa maziwa na mama.

Asifuye mvua imemnyea.

Mvua humnyea asifuye.

Mvua imekunya.

Huku kumenyeshewa sana.  

Mvua imenyesha sana.