Skip navigation

KAZI 1

Kazi ya kusoma

Soma matini kwa makini

Vitenzi vya silabi moja

Hivi ni vitenzi vyenye silabi moja pekee.

Ili kuleta maana kamili, vitenzi hivi huambatanishwa na kiungo KU- katika kauli ya kutenda.

Kama vitenzi vingine, vitenzi vya silabi moja vina maana yaani vinaelezea kuhusu kitendo fulani

  1. -cha - kucha - jua linapochomoza asubuhi k.m kumekucha
  2. -fa - kufa - kuacha kupumua, kupoteza uhai k.m amekufa
  3. -ja- kuja - fika mahali hapa k.m nimekuja
  4. -la- kula - kutia chakula mdomoni k.m anakula
  5. -nya- kunya - kutoa mabaki ya chakula toka tumboni k.m mtoto amekunya
  6. -nywa- kunywa - kutia kinywaji kama vile maji au maziwa mdomoni k.m ninakunywa uji
  7. -pa- kupa - kumkabithi/kumpatia mtu kitu k.m amenipa pesa
  8. -pwa- kupwa - kujaa hadi pomoni - k.m kisima kimekupwa maji
  9. -twa- kutwa - jua linapozama magharibi na usiku kuingia k.m kumekutwa
  10. -wa- kuwa - kutokea katika hali au mahali fulani k.m alikuwa