Shairi - ni utungo wa kisanaa ambao hutumia lugha teule na kushirikisha mpangilio maalum wa maneno ili kuwasilisha ujumbe uliokusudiwa.
Mashairi ya arudhi huzingatia urari wa vina na mizani ilhali mashairi huru hayazingatii urari wa vina na mizani.
Mwanafunzi anatarajiwa kusoma shairi kwa makini ili kung'amua maudhui yaliyomo. Baadhi ya maudhui huwa wazi ilhali mengine yamejifichama.