a) Nomino za Pekee
Ni nomino za vitu au watu walio na maumbile tofauti
Mifano
- Majina ya watu: Petero
- Majina ya mahali: Nairobi
- Majina ya bahari: Bahari Hindu
b) Nomino za Dhahania
Ni nomino za vitu ambavyo ni za kufikirika tu.
K.M;
- Mungu
- Shetani
- Malaika
c) Nomino za Kawaida
Haya ni majina ya wanyama au vitu vyenye umbo.
K.M;
- Shule
- Basi
- Hospitali
d) Nomino za Wingi
Hivi ni vitu ambavyo havihesabiki.
K.M;
- Chumvi
- Maji
- Sukari
e) Nomino za Kitenzi Jina
Ni vitenzi vinavyotumiwa na huchukua nafasi ya nomino katika sentensi.
K.M;
- Kula
- Kuruka
- Kuimba
Tanibihi: Kitenzi jina lazima kiwe mwanzoni mwa sentensi.
K.m.
- Kuimba kwake kulifurahisha.
f) Nomino za Makundi
Hivi hutaja vitu vingi vinavyofikiriwa kama kitu kimoja.
K.M;
- Umati wa watu
- Shada la maua
- Tita la kuni