Skip navigation

HATUA YA PILI

INFORGRAPHIC

HEKAYA

Hekaya ni hadithi ambazo huwa na mhusika mmoja mjanja au mwerefu kuliko wenzake. Mhusika huyu hutumia ujanja kujinufaisha kutoka kwa mhusika mwengine anayedanganyika kwa upesi. Kwa mfano, Hekaya za Abunuwasi, hadithi za sungura mjanja n.k

SIFA ZA HEKAYA

  • Huwa na mhusika mmoja mjanja anayewahadaa wenzake.
  • Mhusika mjanja hunufaika kutoka kwa wengine japo hastahili.
  • Ni hadithi fupi yenye funzo Fulani

UMUHIMU WA HEKAYA

  • Kuburudisha hadhira
  • Kutoa mafunzo
  • Kutahadharisha
  • Kuelekeza na kunasihi
  • Kupitisha muda

KHURAFA

Hurafa au Khurafa ni hadithi ambazo wahusika wake huwa ni wanyama. Hadithi hizi hunuia kuangazia tabia za kibinadamu kupitia kwa wanyama. Hadithi nyingi huwa ni za khurafa ambapo wanyama hupewa uwezo wa kibinadamu wa kuongea, kufanya kazi, kufikiri na nyinginezo.

Kwa kuwa wahusika wote katika hadithi za aina hii ni wanyama kutoka mwanzo hadi mwisho, hatuwezi kusema kwamba mbinu ya uhuishaji/tashihisi imetumika.

SIFA ZA HURAFA

  • Wahusika wake ni wanyama wenye uwezo wa kuongea na kufanya kama binadamu
  • Hurejelea maswala yanayopatikana katika jamii zetu kama utendaji kazi, ukuzaji uchumi, uongozi, utangamano katika jamii, n.k

UMUHIMU

  • Kuburudisha hadhira
  • Kuelimisha watoto kuhusu wanyama mbalimbali na sifa zao
  • Kukuza maadili katika jamii
  • Kuelekeza na kunasihi
  • Kupitisha muda
  • Kukuza maadili na kuburudisha hadhira

MIGHANI

Visakale ni hadithi za mashujaa wanaosifiwa katika jamii. Aghalabu mashujaa hawa walipigania jamii zao katika vita dhidi ya jamii nyingine au vita vya ukombozi. Shujaa katika visakale huitwa jagina. Maadui wa mashujaa huitwa Majahili

SIFA ZA MIGHANI

  • Hutumia chuku kusifia matendo na uwezo wa shujaa.
  • Majagina huwa na uwezo wa ukiamaumbile (uwezo unaozidi wa binadamu)
  • Huwa ni vigumu sana kwa shujaa kuuawa minghairi ya idadi ya maadui wake
  • Shujaa huwa na siri kuu ya nguvu zake (kama nguvu kuwa kwenye kivuli, nywele, n.k)
  • Jagina hupigania haki za jamii yake
  • Jamii ya jagina huwakilisha wema ilhali maadui wao huwakilisha ubaya.
  • Jagina hufa mwishoni, haswa baada ya kusalitiwa na mtu wake.
  • Hadithi hizi huaminika kuwa za kweli ama zenye kiwango fulani cha ukweli; kwamba mashujaa hao walikuwa.

VISASILI

Visasili ni ngano za kihistoria zinazoeleza chimbuko /asili ya jamii/kabila fulani; tamaduni mbali mbali katika jamii ile na namna jamii hiyo ilivyofika katika eneo lake la sasa. Visasili husaidia kuelezea asili ya mambo yasiyoelezekakama vile mauti, jando, tohara, ndoa na tamaduni/imani nyinginezo

SIFA ZA VISASILI

  • Huelezea chimbuko la jamii fulani
  • Matokeo yake hufanyika mwanzoni (k.v mwanzo wa dunia)
  • Aghalabu huhusisha miungu, malaika n.k
  • Kuburudisha