AINA ZA NYIMBO
Nyiso
Hizo ni nyimbo ambazo huimbwa jandoni kwa wavulana na hunyagoni kwa wasichana.Huwavusha vijana kutoka utotoni kuingia utu uzima, hupatikana katika jamii ambazo huthamini tohara.
Umuhimu
a)Hutumiwa kuwandaa kihisia wanaotahiriwa kwa kuwapa ari ya kupitia kijembe cha ngariba.
b)Huwajuza wanaotahiriwa kuhusu majukumu mapya na matarajio ya jamii yao kwao.
c)Huonyesha furaha ya vijana kujivunia hatua ya kutoka utotoni kuingia utu uzima.
d)Huhimiza ujaziri na kukebehi woga.
e)Kuhimiza uzalendo na kuonea fahari utamaduni wa jamii.
f)Kutoa nasaha kwa vijana.
g)Huleta umoja miongoni mwa jamii.
sifo
Nyimbo ambazo hutoa sifa za mtu fulani ambaye ametoa mchango na mafanikio ya watu katika jamii.
umuhimu
a)Husifu matendo chanya ya viongozi au watu mashuhuri katika jamii
b)Hutangaza mafanikio au mchango wa watu wanaosifiwa kwa jamii.
c)Hukuza uzalendo
d)Huweka kumbukumbu au rekodi ya matukio ya kihistoria
e)Huonyesha msimamo na mitazamo ya jamii kuhusu maswala mbalimbali.
f)Hutambua mchango wa watu mbalimbali katika jamii.
mbolezi
Ni nyimbo za kuomboleza.Huimbwa wakati maafa au hafla ya kuadhimisha makumbuzo ya mtu. Pia huimbwa baada ya kushindwa katika michezo au vita.
umuhimu
a)Kusawiri msimamo wa jamii kuhusu kifo
b)Kumbukumbu kwa aliyekufa
c)Hufariji waliofiwa
d)Kutakaza moyo na hisia za aliyefiwa
bembea
Hizi ni nyimbo ambazo huimbwa ili kuwabembeleza watoto walale au watulie wanapolia.Pia huitwa bembelezi au bembejezi.
umuhimu
a)Kutumbuiza na kuongoa watoto
b)Hutumiwa kama sifo
c)Husawiri mfumo wa kiujumi wa jamii husika
d)Husawiri mausiano katika jamii
e)Hukutakaza hisia ambazo muimbaji anaweza kuwa nazo.
f)Huelimisha watoto