Feedback
- Nyiso
- Mbolezi
- Sifo
- Bembea
i.sifa za sifo
a)Husifu na kutukuza watu ambao wamefanya jambo fulani k.m maharusi, wachezaji, wanasiasa n.k
b)Hutumia sitiari kwa ufanifu mkubwa.
c)Hutumia katika miktadha mbalimbali k.v miviga k.m taabili kuwasifu mashujaa waliokufa.
d)Huweza kuimbwa na mtu au watu binafsi wakijisifu
e)Huakisi thamani ya jamii husika.
f)Hupiga chuku sifa za anayesifiwa.
ii. sifa za mbolezi
a)Hutofautiana kutoka jamii moja hadi nyingine na hadhi ya aliyekufa.
b)Huimbwa kwa nia ya kufariji
c)Husifu aliyekufa.
d)Hufungamana na muktadha maalum (matanga)
e)Huimbwa kwa toni ya huzuni
f)Huimbwa kwa mwendo wa utaratibu.
iii.Sifa za bembea
a)Huimbwa taratibu kwa sauti na mahadhi ya chini.
b)Huimbwa na wazazi au walezi wa watoto.
c)Huwa fupi
d)Hutofautiana kutoka jamii moja hadi nyingine
e)Huimbwa kwa kuridiwarudiwa maneno
f)Hutumia lugha shawishi k.v kutolewa ahadi ya zawadi.